ICC: Marekani 'huenda ilitekeleza' uhalifu Afghanistan

Jumba la mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC
Image caption Jumba la mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC

Ripoti ya awali ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, imebaini kwamba jeshi la Marekani na shirika la ujasusi CIA, huenda zilitekeleza makosa ya jinai dhidi ya binadamu nchini Afghanistan.

Ripoti hiyo, iliyotolewa na mwendesha mshataka wa mahakama hiyo Fatou Besouda, inasema kwamba ushahidi wa wafungwa 100 umebaini kwamba walinyanyaswa na kudhulumiwa, huku wengine wakibakwa.

Ripoti hiyo inasema visa vingi vilitokea mwaka 2003 na 2004, japo kuna visa vimeripotiwa miaka 2 ilopita.

Uhalifu sawa na huo unasemekana umetekelezwa katika vizuizi vya siri vinavyosiomamiwa na CIA nchini Poland, Romania, na Lithuania.