Chapisho linalomfananisha bi Obama na 'sokwe' lazua hisia

Bi Michelle Obama
Image caption Bi Michelle Obama

Chapisho la kibaguzi kuhusu mke wa rais wa Marekani Michelle Obama limezua utata unaomuhusu meya wa jimbo la Virginia.

Pamela Ramsey Taylor ,ambaye anaendesha shirika moja la kihisani katika kaunti ya Clay, alimfananisha Michelle Obama na 'sokwe' .

''Itakuwa vyema kuwa na mtu anayefuata mitindo,mrembo na mke wa kwanza mwenye heshima.Nimechoka kuona sokwe lililovaa viatu'',alisema.

Meya mwengine kutoka eneo hilo Beverly Whaling alijibu kwa kusema ''umeifanya siku yangu nzuri''.

Haki miliki ya picha Facebook
Image caption Chapisho la facebook lililomuhusicha bi Obama na sokwe

Bi Beverly Whaling ni meya wa mji wa Clay ambao una idadi ya takriban watu 491.

Mji huo hauna wakaazi wa Marekani wenye asili ya Kiafrika,kulingana na idadi ya watu iliotolewa 2010.

Katika kaunti ya Clay zaidi ya asilimia 98 ya wakaazi 9,000 ni watu weupe.

Licha ya idadi hiyo ndogo katika jimbo hilo ,chapisho hilo la facebook lilisambaa nchini Marekani na katika vyombo vya habari vya kimataifa huku ombi la kuwataka wanawake wote wawili kufutwa kazi likikusanya saini 85,000.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bi Obama akiwa pamoja na mke wa rais mteule wa Marekani Melania Trump

Gazeti la The Washington post na lile la New York Daily yaliripoti kwamba bi Taylor aliondolewa katika wadhfa wake siku ya Jumatatu.