Morsi aondolewa hukumu ya kifo

Mohammed Mosri alihukumiwa kifo Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mohammed Mosri alihukumiwa kifo

Mahakama nchini Misri imebatilisha hukumu ya kifo aliyopewa rais aliyepinduliwa Mohammed Morsi.

Morsi alikumiwa kifo baada ya kulaumiwa kuhusika na kutoroka kwa wafungwa wengi wakati wa mapinduzi ya mwaka 2011.

Alichaguliwa kuwa rais mwaka 2012 lakini akaondolewa na jeshi mwaka mmoja baadaye, kufuatia maandamano makubwa ya kupinga utawala wake.

Morsi ashahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa mashtaka yanayohusu ugaidi na bado anakabiliwa na mashtaka kwa makosa mengine.