Rawlings alishtaki gazeti kwa kumchafulia jina

Jerry Rawlings aliitawala Ghana kwa miaka 18 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jerry Rawlings aliitawala Ghana kwa miaka 18

Aliyekuwa rais wa Ghana Jerry Rawlings, amelishtaki gazeti moja lenye makao yake nchini Marekani la Africawatch, baada ya gazeti hilo kuripoti kuwa bwana Rawlings, alikuwa ameugua ugonjwa wa kutetemeka wa Parkinson.

Kesi hiyo imepelekwa mahakamani mjini Accra na mawakili wa rais huyo wa zamani, ambao wanasema kuwa gazeti la Africawatch, limemchafulia jina bwana Rawlings, na wala halikuthibitisha taarifa hiyo kabla ya kuichapisha.

Jitiha kadha za kulifikia gazeti hilo kulijulisha liiondoe taarifa hiyo hazijafua dafu.

Bwana Rawlings aliingia madarakani mwaka 1979 kwa njia ya mapinduzi na kuitawala Ghana kwa miaka 18.