Meneja: Pesa ziliwasili kwa ndege mbili, tukazihesabu kwa siku 10

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jumla ya naira bilioni 1.2 ziliwasili kwa ndege mbili

Meneja mmoja wa benki nchini Nigeria, anasema kuwa iliwachukua wafanyakazi wa benki siku kumi, kuhesabu pesa zote zilizopelekwa kwenye benki hiyo na msaidizi wa gavana wa jimbo la Ekiti

Msaidizi huyo Abiodun Agbele, anachunguzwa na shirika la kupambana na ufisadi nchini Nigeria.

Pesa zote ambazo ni dola milioni 3.9 au bilioni 1.2 katika sarafu ya Nigeria ya naira, ziliwasili kwa ndege mbili kwa mujibu wa meneja wa benki.:

Meneja huyo wa benki ya Zenith, anasema kuwa bwana Agbele alimuambia atume pesa hizo kwa akaunti tofauti.

Hata hivyo anasema hakuripoti suala hilo kuwa la kutiliwa shaka kwa sababu haukuwa wajibu wake afanye hivyo.

Kwa mujibu wa shirika la kupambana na ufisadi nchini Nigeria, bwana Agbele anakumbwa na mashtaka ya kupora pesa kutoka kwa ofisi ya mshauiri wa zamani wa masuala ya usalama wa kitaifa Sambo Dasuki.