Ndayisenga ashinda awamu ya pili ya Tour of Rwanda

Valens Ndayisenga anayechezea timu ya Dimension Data ya Afrika kusini
Image caption Valens Ndayisenga anayechezea timu ya Dimension Data ya Afrika kusini

Mnyarwanda Valens Ndayisenga anayechezea timu ya Dimension Data ya Afrika kusini ndiye mshindi wa raundi ya pili ya mashindano ya kimataifa ya mbio za baiskeli Tour of Rwanda yanayoendeleea nchini Rwanda.

Umati wa watu ukishangilia Valens Ndayisenga aliyeingia mjini Karongi akiwa wa Kwanza akitumia muda wa saa 3 dakika 16 na sekunde 46. Alimuacha nmashindano ya kimataifa ya mbio za baiskeli Tour of Rwanda yuma kwa dakika moja Kangangi Suleiman wa Kenyan Riders Downunder na Areruya Joseph aliyeshika nafasi ya tatu.

Kwa furaha isiyo kifani, Ndayisenga anayechezea timu ya Dimension Data ya Afrika kusini amesema leo ilikuwa siku ya kujituma sana kutokana na mbio hizi sasa kuhamia milimani:

Amesema, "Ziliposalia kilomita 10 tumetumia nguvu nyingi. Mbele yetu kulikuwa wachezaji wakubwa na wenye majina: Bosco ,Areruya na waEritrea watatu ,lakini ,nimefanya shambulio kubwa wakachoka ndivyo nilivyowapiku"

Image caption Mashindano ya kimataifa ya mbio za baiskeli Tour of Rwanda

Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Rwanda Felix Sempoma amesema ushindi wa Valens Ndayisenga hata kama anachezea Dimension Data ya Afrika kusini una maana kubwa kwa Rwanda katika kuwania taji la afrika:

"Hata kama ni mchezaji wa Dimension Data lakini ni Mnyarwanda na kwa hiyo alama zake kama ataibuka na ushindi wa Tour of Rwanda ,zitakuwa alama za taifa la Rwanda na tutapanda kiwango"

Coacha Sempoma amesisitiza kuwa bado ni mapema mno kuzungumzia taji la Tour of Rwanda kwani bado ni mapema mno.

Image caption Mashindano ya kimataifa ya mbio za baiskeli Tour of Rwanda

Valens Ndayisenga ndiye mshindi wa mbio hizi miaka miwili iliyopita.Kwa ujumla nafasi tatu za kwanza zinashikiliwa na wanabaiskeli wa Rwanda.

Valens Ndayisenga ambaye amevikwa jezi ya manjano anamzidi kwa dakika 1 na sekunde 25, Areruya Joseph wa pili huku bingwa mtetezi Jean Bosco Nsengimana akiwa kwenye nafasi ya tatu.

Image caption Mashindano ya kimataifa ya mbio za baiskeli Tour of Rwanda

Wote wanafwatiwa kwa karibu na bingwa wa afrika Okumariam Tesfom ambaye yuko katika nafasi ya nne,mwanabaiskeli wa kwanza anamzidi dakika 1 na sekunde 32.

Kesho washindani watatoka hapa mjini Karongi na kwelekea katika mji wa Rusizi umbali wa kilomita 115.