Trump: Majina ya wakuu ayajuaye ni mimi

Donald Trump Haki miliki ya picha Reuters

Rais mteule wa Marekani Donald Trump ametetea utaratibu wa mpito nchini humo na kusema hakuna mzozo kinyume na inavyotangazwa kwenye vyombo vya habari.

Bw Trump ameandika kwenye Twitter kwamba shughuli ya kuwachagua mawaziri wake inaendelea "kwa mpango" na kwamba ni yeye pekee awajuaye watu watakaoteuliwa.

Mbuneg wa zamani, Mike Rodgers, aliyekuwa akisimamia masuala ya usalama wa taifa katika kundi la mpito amejiuzulu.

Kumekuwa na taarifa kwamba alisukumwa nje na shemejiye Bw Trump.

Taarifa katika vyombo vya habari zimedokeza kwamba kuna mzozo mkali miongoni mwa maafisa wanaosimamia shughuli ya mpito upande wa Bw Trump, ambao makao makuu yao yamo katika jumba la Trump Tower, New York.

Meya wa zamani wa New York, Rudolph Giuliani, ambaye anatarajiwa kupewa wadhifa mkuu, amesema shughuli ya mpito huwa ngumu na ni kawaida kukumbwa na matatizo madogo hapa na pale.

Bw Trump ataapishwa kuwa rais 20 Januari mwaka 2017.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii