Korea Kaskazini yamtaja Trump kwa mara ya kwanza

Trump na Obama Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bw Trump na Obama

Kituo cha habari cha serikali,cha Korea Kaskazini kimemrejelea kwa mara ya kwanza rais mteule wa Marekani Donald Trump ingawa kwa njia isiyo ya moja kwa moja.

Kituo hicho cha serikali kwa ufupi kilimtaja Bw Trump katika mkutano wa wahariri kwa kumkosoa rais wa Korea kusini, Park Guen-Hye.

Mkutano huo ulikuwa ukiangazia ukakamavu wa Bi Park kuhusiana na ''mfumo wa dharura wa Trump''.

Licha ya nchi hiyo kuvidhibiti vituo vya habari bado hawajatangaza rasmi habari za ushindi wa Trump wiki moja iliyopita, ikilinganishwa na mwaka 2008 ambapo vilichukua siku nne kumtangaza rasmi rais Barack Obama.