Mjenga misuli ala kondo la nyuma la mpenziwe

Wajenga misuli, Australia Haki miliki ya picha AP
Image caption Wajenga misuli, Australia

Mjenga misuli ambaye alipata umaarufu kwenye mtandao baada ya kuchoma na kula kondo la nyuma la mpenzi wake amesema kondo hiyo lililokuwa kama maini.

Mwamume huyo mwenye umri wa miaka 32 kutoka Australia amesema atakuwa 'makini' jinsi kondo hiyo ingeonja.

''Mpenzi wangu hakuwa na shida nami kula nyama hiyo, lakini nilipoianza kuichoma jikoni, sidhani alipenda, Aaron Curtis amesema.

''Haikuwa na ladha tofauti lakini ngozi yake ilinikumbusha maini.''

Wakati wa uja uzito, kondo la nyuma husambaza chakula kutoka kwa mama hadi kwa mtoto.

Kwa mzazi kula kondo hiyo, baada ya kujifungua, si jambo la kushangaza kwamba kondo hiyo ina virutubisho vya kiasili.

Nimekuwa na maoni tofauti kuhusiana na kutupa chakula, kwa hivyo ulaji wa kondo hiyo halikuwa jambo kubwa kwake , amesema Aaron.

Nimekuwa na wiki nzuri katika mazoezi yangu baada ya kula kondo hiyo igwaje usingizi wangu umekuwa ukitatizwa na jukumu la ubadilishaji nepi.