Kwa nini Trump hataendesha gari tena

Gari la Trump Haki miliki ya picha Getty Images

Rais mteule wa Marekani Donald Trump, ambaye ataingia madarakani Januari mwaka ujao, anamiliki magari mengi ya kifahari.

Hata hivyo, hataweza kuyaendesha tena chini ya sheria za sasa.

Rais na marais wa zamani hawaruhusiwi kuendesha magari katika barabara za umma nchini Marekani.

Badala yake, huwa magari yanayowabeba yanaendeshwa na maafisa wa Secret Service.

Hali ni hiyo hiyo kwa makamu wa rais.

Makamu wa rais wa sasa Joe Biden hata hivyo alifanikiwa kuendesha gari lake alipendalo aina ya 1967 Corvette kwenye kipindi cha Garage cha Jay Leno, kwa kuendesha gari katika barabara za serikali chini ya ulinzi.

Magari yanayomilikiwa na Bw Trump, ambayo hatapata fursa ya kuyaendesha karibuni kwa mujibu wa Gearheads.com, ni:

  • 2003 Mercedes-Benz SLR McLaren
  • 1956 Rolls-Royce Silver Cloud (taarifa zinasema ni moja ya magari ya kwanza aliyoyanunua Trump)
  • 2011 Chevy Camaro Indy 500 Pace Car
  • Na pikipiki aina ya Orange County Chopper ya rangi ya dhahabu

.

Mada zinazohusiana