Pacha waliotungwa siku tofauti Australia

Mapacha hawa walitungwa siku tofauti Haki miliki ya picha SEVEN NETWORK
Image caption Mapacha Charlotte na Olivya

Mwanamke raia wa Australia aliyeambiwa na madaktari kuwa hawezi kutunga mimba amejifungua pacha wanaodaiwa kutungwa siku tofauti.

Kate Hill alikua akipokea matibabu ya kumuwezesha kutunga mimba.

Wakati wa matibabu hayo alitunga mimba za mapacha walioachana kwa siku kumi. Hatua kama hii huwa ni nadra sana na watafiti wanaiita 'Superfestation', ambapo mwanamke huweza kutunga mimba nyingine wakati tayari akiwa mja mzito.

Haki miliki ya picha SEVEN NETWORK
Image caption Kate Hill na Mumewe Peter Hill wazazi wa mapacha hao

Mapacha hao wasichana, Charlotte na Olivia wana miezi kumi sasa lakini walizaliwa na uzito tofauti na hata maumbile.

Kate Hill amesema waligundua maajabu ya wana wao baada ya kuzaliwa.

Katika hali hiyo inayojulikana kama 'superfestation', mwanamke huendelea kupata hedhi hata haada ya kutunga mimba na ndio maana Bi Hill alitunga mimba baada ya siku kumi za uja uzito wa kwanza.

Ni visa kumi tu vimenakiliwa duniani vya watoto waliozaliwa kwa mazingira sawa na mapacha hawa.