Harusi ya dola milioni 74, yazua hasira

Mwanasiasa huyo ametumia dola milioni 74 kugharmia harusi ya bintiye Haki miliki ya picha JANARDHANA REDDY FAMILY
Image caption Bwana Reddy, Bibi Harusi na familia ya bwana harusi

Harusi moja ya kifahari nchini India ya binti ya mwansiasa mmoja imezua ghadhabu ya umma, kutokana na gharama yake wakati mamilioni ya raia wakiwa maskini.

Harusi hiyo iliyofanyika kwa siku tano ilifadhiliwa na mwekezaji mashuhuri ambae pia alikua Waziri katika jimbo moja India, G Janardhana Reddy.

Mwanasiasa huyo aliandaa kwa heshima ya binti yake aliyekua bibi harusi bi, Brahmani na iligharimu dola milioni 74.

Kadi za mwaliko ziliremebeswa kwa dhahabu, huku wageni wakitumbuizwa na wasanii kutoka Bollywood.

Watu wengi wamelalamikia harusi hiyo kama kejeli kwa masikini na onyesho la utajiri.

Ilifanyika wakati serikali ya India ilipotangaza kuondoa sarafu ya rupee ya 500 na 1000 kama hatua ya kuchunguza mali iliyopatikana kwa njiya isiyo halali.

Mamilioni ya raia wa India wamekua wakipiga foleni kubadilisha sarafu zao na wengi wamelalamikia hatua ya serikali.Harusi nchini India huwa za kifahari na gharama zote hulipiwa kwa pesa taslimu.

Bwana Reddy ametetea heshima yake kwa bintiye akisema ilimbidi kuuza baadhi ya mali zake zilizoko, Bangalore na Singapore ili kugharamia harusi hiyo. Aidha amesema malipo yote yalifanyika miezi sita kabla ya harusi kufanywa.

Haki miliki ya picha JANARDHANA REDDY FAMILY
Image caption Hekalu zimerembeshwa, kwa mitindo ya Bollywood

Licha ya kujitetea , raia wengi wamelalamikia kwenye mitandao ya kijamii.

Baadhi ya wakosoaji wa serikali wametaka chama tawala cha Waziri Mkuu Narendra Modi cha 'Bharatiya Janata Party' {BJP}, kuwachunguza wanachama wake dhidi ya ufisadi.

Bwana Reddy aliwahi kufungwa jela miaka mitatu kwa makosa ya ufisadi. Aliachiwa huru kwa dhamana mwaka uliopita. Hekalu ambapo harusi hiyo iliandaliwa zilirembeshwa kwa dhahabu na michoro maalum iliyotungwa na waandaa filamu kutoka Bollywood.

Kuna magari maalum ya kifahari pia iliyowasafirisha wageni waalikwa.

Harusi ghali zaidi duniani

Hapa ni baadhi ya harusi ghali zaidi duniani:

  • Vanisha Mittal, bintiye mtu wa pili kwa utajiri India Lakshmi Mittal, alimuoa Amit Bhatia katika sherehe iliyogharimu $74m mwaka 2004.
  • Harusi ya Mwanamfalme Charles na Diana wa Uingereza mwaka 1981 iligharimu £30m ($37.2m), kwa fedha za sasa ni karibu £116m. Harusi ya mwana wao William na Kate Middletoniligharimut £20m, according to the Daily Mail.
  • Harusi ghali zaidi ilifanyika Urusi mwezi Machi, kati ya mwana wa bilionea Said Gutseriev aliyemuoa Khadija Uzhakhovs mjini Moscow. Alitumia $1.2m kwa mavazi ya harusi pekee. Wageni walitumbuizwa na watu wanamuziki watatu mashuhuri: Jennifer Lopez, Sting na Enrique Iglesias. Gharama ilikuwa dola bilioni kadha.