Urusi yajiondoa katika harakati za kujiunga na ICC

Vladmir Putin
Image caption Vladmir Putin

Urusi inajiondoa katika harakati za kujiunga na mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC

Wizara ya maswala ya kigeni imesema kuwa mahakama hiyo imeshindwa kutimiza mahitaji na haijawahi kuwa huru.

Imesema kuwa haifurahii uchunguzi wa ICC unaondelea kuhusu vita vya muda mfupi kati ya Urusi na Georgia miaka minane iliopita,ikisema kuwa mahakama hiyo ilipuuza uchokozi wa Georgia .

Wiki hii mahakama hiyo imetaja matukio ya mwaka 2014 katika eneo la Crimea kama vita kati ya Urusi na Ukraine,hatua inayomaanisha kuwa eneo hilo sasa litasimamiwa na mahakama ya ICC.