Wataalam wataka makaburi ya albino kulindwa

Mtu mwenye ulemavu wa ngozi
Image caption Mtu mwenye ulemavu wa ngozi

Mtaalam wa maswala ya watu wenye ulemavu wa ngozi ameambia BBC kwamba miili ya watu hao iliozikwa inendelea kufukuliwa kwa lengo la kuchukua viungo vyao.

Watu wanaoishi na ulemavu huo tayari wanashambuiwa kutokana na imani potofu kwamba wana nguvu maalum na kwamba viungo vyao vya mwili vinaweza kutumika kama dawa za miujiza.

Zaidi ya albino 600 wameuawa katika mataifa tofauti nchini Afrika tangu mwaka 2007 kutokana na mila potofu.

Sasa mtaalamu huyo Ikponwosa Ero anasema kuwa miili iliozikwa pia inalengwa.

Alikuwa akizungumza katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye ulemavu wa ngozi uliofanyika kando kando ya mji wa Nairobi ambao uliwaleta pamoja wawakilishi kutoka mataifa 15.

Visa vingi vimeripotiwa nchini malawi,Mozambique na Tanzania ambapo albino wengi wanashambuliwa sana.

Waliohudhuria wametaka makaburi ya albino kufunikwa na saruji ili kuzuia ufukuaji.