FIFA yamuadhibu Saoud al-Mohannadi

Qatar Haki miliki ya picha Google
Image caption Saoud al-Mohannadi

ofisa mmoja wa soka kutoka nchini Qatar, ambao ndiyo wenyeji wa kombe la dunia linalotarajiwa kufanywa mwaka 2022, amepigwa marufuku katika shughuli zozote zinazohusiana na mpira wa miguu kwa muda wa mwaka mmoja kwa kukataa kutoa ushirikiano kama shahidi katika uchunguzi unaoendelea.

Msemaji wa kamati ya nidhamu ya FIFA ,na shirikisho la soka la kimataifa walisemema kuwa afisa huyo hakuweza kutoa maelezo ya kutosha kwa hofu ya kuhatarisha kesi, ofisa huyo Saoud al-Mohannadi, pia alipigwa faini inayokadiriwa kufikia dola za kimarekani elfu ishirini