Meya wa New York aeleza hofu ya jamii za Wahamiaji kuhusu Trump

Meya wa New York Bill de Blasio Haki miliki ya picha AP
Image caption Meya wa New York Bill de Blasio

Meya wa New York kutoka chama cha Democratic, Bill de Blasio amesema kuwa amemwambia Donald Trump kwamba jamii za wahamiaji katika mji huo zinahofia juu ya hatua atakazozichukua dhidi yao.

Bwana Trump ametishia kuwarejesha makwao ama kuwafunga wahamiaji milioni tatu wenye historia ya uhalifu.

Mameya wa miji mingine ikiwemo Los Angeles na Washington wamesema kuwa watawalinda watu dhidi ya kurejeshwa walikotoka.