Valens Ndayisenga aendelea kuongoza Tour du Rwanda

Image caption Valens Ndayisenga anaendelea kuongoza

Valens Ndayisenga Mnyarwanda anayechezea timu ya Dimension Data ya afrika kusini, bado anaendelea kushika usukani wa mbio za baiskeli za Tour du Rwanda, na tayari ameshaweka muda wa dakika 1 na sekunde 16 kati yake na Areruya Joseph anayeshika nafasi ya pili.

Hii leo kundi la wanabaiskeli 22 likiongozwa na Mnyarwanda Areruya Joseph limevuka mstari wa mwisho kwa kutumia muda ulio sawa wa saa 4 dakika 2 nukta 43, japo ushindi wa awamu hii ya kilimita 140 umepewa kijana Areruya Joseph wa timu ya Rwanda kwa kuwazidi tu taili la baiskeli:

Image caption Mashabiki waliojitokeza kutizama mashindano

Miongoni mwa waliomaliza katika kundi hilo la kwanza ni Mkenya Kangangi Suleiman wa timu ya Kenya Riders Downunde ambaye hata katika awamu ya pili alifanya vyema kwa kumaliza kwenye nafasi ya pili.

Upande wa timu bado Dimension Data ya afrika kusini iko kileleni kwa kuwa na kikosi cha wachezaji mchanganyiko wa wanyarwanda na wa Eritrea.

Kesho katika siku ya sita ya mashindano haya washindani watatoka mjini Huye na kuelekea Kaskazini kwenye mji wa Musanze umbali wa kilomita 125.