Lori lalipuka na kuua zaidi ya watu 70, Msumbiji.

Lori laua kadhaa Msumbiji
Image caption Lori laua kadhaa Msumbiji

Zaidi ya watu 70 wamekufa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa baada ya Lori la mafuta kulipuka nchini Msumbiji.

Kwa mujibu wa serikali ya nchi hiyo, watu walikuwa wakinyonya mafuta wakati lilipolipuka.

Taarifa nyingine zinasema kuwa lori hilo lilipinduka. Tukio hilo limetokea katika jimbo la Tete karibu na mpaka wa nchi hiyo na Malawi.

Serikali imetuma timu ya wataalamu katika eneo hilo kuchunguza zaidi chanzo cha ajali na kusaidia majeruhi.