wadau wa mazingira wakutana Morocco

Morocco
Image caption Waandamanaji wakitaka juhudi zaidi katika kupambana na joto duniani.

Wajumbe wanaohudhuria mkutano mkubwa wa kimataifa juu ya mabadiliko ya tabia nchi wanakutana mjini Marrakech, nchini Morocco, wametoa wito kwa viongozi wa ngazi za juu wa kisiasa kuonesha dhamira ya dhati katika kupambana na suala hilo.

Wajumbe hao wanakutana huku kukiwa na wasiwasi mkubwa kwamba rais mteule wa Marekani, Donald Trump, anaweza kujaribu kurudisha nyuma ahadi na jukumu la nchi yake ya kukataa gesi chafu.

Ujumbe huo umesifu kasi ya hali ya juu iliyooneshwa mwaka huu juu ya mipango ya kupunguza uzalishaji wa gesi chafu kimataifa, Pamoja na hayo wametoa wito wa hatua za haraka kuchukuliwa ili kuongeza matarajio, wakisema kuwa suala hili lilipaswa kutiliwa mkazo kitambo kilichopita tangu kufanyika kwa mkutano wa Paris .

Makubaliano ya mkutano huo yalikuwa na lengo la kupunguza joto duniani mpaka kufikia mwishoni mwa karne hii mpaka kufikia nyuzi joto mbili zaidi ya hapo itahesabiwa kuwa ni hali ya hatari.