Chaka, kijiji cha mbali kilichopoteza watu wengi Mandera, Kenya

Chaka, kijiji cha mbali kilichopoteza watu wengi Mandera, Kenya

Kenya inapokabiliana na mashambulio ya kigaidi ya mara kwa mara, kuna kijiji kimoja kati kati mwa nchi hiyo kilichoathiriwa zaidi na mashambulio ya kigaidi Mandera.

Wakaazi wa mji wa Chaka umewapokea vijana wake wengi kwenye mifuko ya kusafirishia maiti baada ya kuuawa na wapiganaji wa al-Shabaab katika mji huo unaopatikana kaskazini mashariki mwa Kenya.

Vijana hao walikwenda huko kufanya kazi ya kuchimba mawe.

Al shabaab walitoa onyo kwa wasiokuwa wenyeji asili wa Mandera waondoke mji huo wa kaskazini mashariki la sivyo wauawe.

Dayo Yusuf amesafiri mkoa wa kati Kenya, kujua vijana hao wamepokea vipi vitisho hivyo.