Msukosuko washuhudiwa Kinshasa, DRC

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polisi wa kukabiliana na maandamanoa wamepelekwa kwenye mitaa ya Kinshasa

Ripoti kutoka Jamhuri ya Demokrasi ya Congo zinasema kuwa kuna msukosuko mkubwa, huku vikosi vya usalama vikitumwa kwenda mji mkuu Kinshasa, baada ya utawala kupiga marufuku mkutano wa upinzani.

Walioshuhudia wanasema kuwa maafisa wa Umoja wa Mataifa nao pia wanazuiwa kufika kwa nyumba ya mwanasiasa wa upinzani, Etienne Tshisekedi.

Ametoa wito kwa rais Kabila kuondoka madarakani wakti muhula wake utakamilika mwezi ujao.

Bwana Kabila amesema kuwa uchuguzi huo wa mwezi Disemba ni lazima uhairishwe na amemteua mwanasiasa wa upinzani Samy Badibanga kuwa waziri mkuu mpya.