Washukiwa wa al Shabab wauawa Kenya

Haki miliki ya picha AP
Image caption al Shabab ndilo kundi hatari zaidi nchini Somalia

Mamlaka nchini Kenya zinasema kuwa polisi wameua watu wane, wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Kiislamu, karibu na mpaka wa Somalia, na hivyo kuzuwia kile wanachosema, kuwa shambulio lilopangwa kufanywa katika kituo cha polisi.

Afisa wa wilaya Mohammed Saleh, alisema polisi walipata bunduki, simu za mkononi na makoti ya jeshi la Somalia, baada ya kuwavizia na kushambulia wanaume hao, katika wilaya ya El Wak, huko Mandera.

Alisema hao walikuwa kati ya watu 20 wanaoshukiwa ni wafuasi wa al Shabaab, kundi lilosema litalipiza kisasi kwa wanajeshi wa Kenya kuwa Somalia.