Dela, Mkenya aliyevuma kupitia wimbo wa Adele

Dela, Mkenya aliyevuma kupitia wimbo wa Adele

Kwa wapenzi wa mziki wa taratibu, Adele ambaye ni msanii kutoka hapa Uingereza na ni maarufu kote duniani, basi kibao chake cha Hello bila shaka wengi mlikisikia na kuvutiwa nacho.

Hata hivyo baada ya kibao hicho kutolewa, watu wengi kutoka nchi mbalimbali walianza kuiga wimbo huo kwa lugha zao.

Adeline Maranga, maarufu kwa jina la Dela kutoka Kenya aliwavutia wengi kwa kuimba wimbo huo kwa lugha ya Kiswahili.

Zuhura Yunus alizungumza naye, mwanzo kujua mziki wake ni wa aina gani.