Mlipuko wa ugonjwa wa kimeta wadhibitiwa Tanzania

Mlipuko wa ugonjwa wa kimeta wadhibitiwa Tanzania

Mlipuko wa ugonjwa wa kimeta uliotokea katika hifadhi ya taifa nchini Tanzania na kuuwa takriban wanyama pori mia moja na thelathini hatimae umedhibitiwa.

Kulikuwa na wasiwasi kuwa ugonjwa huo unaweza kusambaa kwa binadamu kwani wafugaji waliopoteza mifugo yao, iliaminiwa walikuwa wakila mizoga ya wanyama waliokufa.

Mlipuko huo ulitokea katika njia wapitao wanyama kaskazini mwa Tanzania mbugani Selela, eneo ambalo ni maarufu kwa utalii.

Kutoka huko Aboubakar Famau ana taarifa zaidi.