Wanaume wafungwa uzazi kwa pamoja Kenya

Wanaume wafungwa uzazi kwa pamoja Kenya

Wanaume karibu mia moja jijini Nairobi, Kenya walifanyiwa upasuaji wa kukata na kufunga mirija yao ya uzazi kama njia ya kupanga uzazi kwa pamoja. Njia hiyo ya upangaji uzazi kwa Kiingereza hufahamika kama Vasectomy.

Walifanyiwa upasuaji kwenye ukumbi wa taifa wa sanaa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya upangaji uzazi kwa njia hiyo ya Vasectomy duniani.

Mwandishi wa BBC Abdinoor Aden anaarifu zaidi.