Mwanamke mweusi aliyekabili polisi Marekani
Mwanamke mweusi aliyekabili polisi Marekani
Mwezi Julai, Ieshia Evans, alishiriki maandamano ya Black Lives Matter Baton Rouge, Louisiana.
Mwanamume mmoja aliposema hawakufaa kuwa barabarani wakiandamana, alimjibu: "Tuko hapa tufanye nini?"
Picha yake akiwa amesimama bila kuonekana kubabaika mbele ya maafisa wa polisi ilisambaa sana duniani. "Naipenda picha hiyo, kuna nguvu za mwanamke hapo, nguvu za mtu mweusi,” anasema.
"Wanaume wetu weusi wanaweza kujua malkia wao wanasimama nao - hawajaachwa peke."