Waliopoteza mali wakati wa maandamano Ethiopia kusaidiwa kujiinua

Waliopoteza mali wakati wa maandamano Ethiopia kusaidiwa kujiinua

Baadhi ya biashara za kigeni ambazo ziliteketezwa katika maandamano dhidi ya serikali mwezi uliopita nchini Ethiopia sasa zimerejelea shuguli zao.

Maandamano hayo yalifuatia vifo vya zaidi ya watu hamsini katika mkanyagano kwenye sherehe za kidini za kila mwaka katika jimbo la Oromia.

Waandamanaji walilenga biashara katika majimbo mawili makubwa zaidi nchini humo, na kuilazimisha serikali kutangaza miezi sita ya hali ya hatari.

Lakini sasa kamati inayoshugulikia uwekezaji nchini humo inasema iko tayari kuzisaidia biashara hizo kuinuka tena. Emmanuel Igunza ana maelezo zaidi kutoka Addis Ababa.