Lucy Quist: Mkuu wa kampuni ya Airtel Ghana

Lucy Quist: Mkuu wa kampuni ya Airtel Ghana

Lucy Quist, ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Ghana Ltd. Anasema kwa watu wengi, kuongozwa na mwanamke bado ni jambo geni.

"Kwa hivyo, hiyo ina maana kwamba lazima niweze kwenda walipo, kwa sababu ndipo tufanikiwe pamoja, nahitaji kuukubali kiasi mtazamo wao,” anasema.

Angependa dunia ifike pahala ambapo muhimu sana haitakuwa kuhusu wanawake wanaofanya mapya, bali wanawake wengi wanaofanya mambo wafaayo kuyafanya.