India yaapa kulipiza kisasi cha wanajeshi wake waliouawa Kashmir

Wanajeshi wa India Haki miliki ya picha AP
Image caption Uhusiano baina ya India na Pakistan umekuwa mbaya katika miezi ya hivi karibuni

Jeshi la India limeapa kulipiza kisasi kwa mauaji ya wanajeshi wake watatu katika jimbo linalozozaniwa la Kashmir huku hali ya wasi wasi ikiendelea kutanda baina ya nchi hiyo na Pakistan.

Wapiganaji kutoka Pakistan waliwateka wanajeshi wa India na kukata viungo vya mmoja wao , limesema jeshi.

Pakistan inasema takriban raia 9 wa upande wake wa mpaka waliuawa na wengine 7 kujeruhiwa Jumatano asubuhi wakati wakati bomu kutoka india lilipopiga basi la abiria.

Nchi zote mbili zinashutumiana kwa kuvunja makubaliano ya mwaka ya Kashmir ya 2003.

Makumi ya raia na wanajeshi wa kila upande wameuawa tangu yaanze mashambulio ya wanamgambo wa dhidi ya ngome ya kijeshi ya India mwezi wa Septemba.

Afisa wa jeshi la India Iameliambia shirika la habari la India -Press Trust kwamba "msafara wa kikosi doria cha India cha kukabiliana na na ugaidi kilitekwa na magaidi kabla ya kujenga ngome katika eneo la udhibiti wake kwenye uzio wa msitu katika eneo la Machil lililopo wilayani Kapwara " Jumanne.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Pakistani amekanusha madai hayo.

Image caption Kutokana na shambulio hilo, kulikuwa na ufyatuaji mkubwa wa risasi na ulipuaji mabomu kutoka kila upande kwenye eno hilo

V"ulipizaji kisasi utakuwa mzito kwa kitendo hiki cha uoga," Alisema msemaji wa jeshi la India Kanali Rajesh Kalia.

Kutokana na shambulio hilo, kulikuwa na ufyatuaji mkubwa wa risasi na ulipuaji mabomu kutoka kila upande kwenye eno hilo.

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Kumekuwa na maandamano ya miezi kadhaa ya wakazi wa Kashmir wenye hasira dhidi ya utawala wa India

..Nchi zote mbli India na Pakistan zinadai walislam wa Kashmir ndio walio wengi , lakini wanadhibiti sehemu tu ya jimbo hilo.

Mzozo wa mpaka baina ya nchi mbili umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya miongo sita, na katika vita viwili kati ya vitatu silaha za nuklia zilitumiwa na majeshi yanayohasimiana vilikuwa ni kuhusu Kashmir.

Kila unapoibuka mzozo katika jimbo la Kashmir, hofu ya wengi ni kwamba unaweza hatimae kuongezeka na kuwa makabiliano makubwa baina ya nchi hizo mbili zenye nuklia.

Lakini wachambuzi bado wanaamini kuwa huenda hilo lisitokee na kwamba makabiliano ya hapa na pale na mzozo wa kidiplomasia wa pande mbili una uwezekano mkubwa wa kuendelea.