Rais wa Korea Kusini alinunua dawa za Viagra

Park Geun-hye
Image caption Park Geun-hye

Kashfa nchini Korea Kusini inayohusisha maisha ya faragha ya rais Park Geun-hye imechukua mwelekeo usio wa kawaida huku ikidaiwa kuwa afisi yake ilinunua dawa nyingi za kuongeza nguvu za kiume Viagra .

Msemaji wa serikali amesema kuwa takriban dawa 400 zinazotumiwa kutibu tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume zilinunuliwa kukabiliana na ugonjwa unaosababishwa na tofauti ya hali ya anga Afrika mashariki,ijapokuwa dawa hizo hazikutumika.

Hayo yanajiri huku kukiwa na shutuma kwamba kiongozi huyo wa Korea Kusini aliruhusu urafiki mrefu kushawishi maamuzi yake kuhusu maswala ya kitaifa na kile rais huyo alichovaa.

Image caption Waandamanaji wakipinga uongozi wa rais Park Geun Hye

Afisi ya rais imethibitisha ilinunua dawa 364 za viara na dawa nyengine kama hizo ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa katika ziara ya Afrika mashariki,ijapokuwa dawa hizo hazikutumika.

Mwandishi wa BBC Evans aiyepo mjini Seoul anasema kuwa ugunduzi huo utazidisha lawama zinazomkabili rais huyo .

Wakorea wengi wanaamini kwamba bi Park anaishi katika maisha tofauti swala ambalo litaongeza shinikizo za kisiasa kwa yeye kujiuzulu.

Image caption Dawa za Viagra zilizonunuliwa na afisi ya rais huyo wa Korea Kusini

Uvumi wa awali miongoni mwa raia wa Korea unadai kuwa bi Park huenda alihusika na ibada ya kimila na rafikiye bi Choi.

Bi Choi ambaye ni rafiki wa muda mrefu wa bi Park ni mwana wa Choi tae-min kiongozi wa kidini ambaye alihusishwa na babake bi Park aliyekuwa rais Park Chung -hee.

Image caption Ushahidi uliobaini kwamba dawa hizo zilinunuliwa