Ukame watishia maelfu ya watu Malawi

Ukame watishia maelfu ya watu Malawi

Zaidi ya raia wa Malawi milioni sita na nusu wanakabiliwa na njaa na uhaba mkubwa wa chakula baada ya kipindi kirefu cha ukame. Biashara kubwa na ndogo zimeathirika vibaya na ukosefu wa maji na umeme.

Mpango wa chakula duniani unaonya kuwa tatizo hilo linaweza kuongezeka zaidi kuelekea mwishoni mwaka ikiwa misaada ya kibinadamu haitaongezwa.

Malawi ni nchi iliyoathirika vibaya zaidi katika eneo la kusini mwa Afrika na zaidi ya robo tatu ya watu wake wanaihitaji msaada wa chakula.

Mwandishi wetu Anne Soy ana taarifa zaidi.