Msongamano mkubwa wa magari Los Angeles

Msongamano mkubwa wa magari Los Angeles

Video ya foleni ndefu ya magari kusini mwa jimbo la California nchini Marekani imevuma sana mtandaoni, wengi wakisema huenda ndiyo foleni mbaya zaidi duniani.

Video hiyo ilipigwa kwa kutumia helikopya ya shirika la habari na inaonesha magari yakiwa yamekwama katika barabara nambari 405 katika mji wa Los Angeles Jumanne.

Wengi wa wakazi walikuwa wanakimbia nyumbani kuhudhuria sherehe za Siku ya Shukrani, moja ya siku zinazoenziwa sana Marekani.