Nyota wa filamu India abeba nguruwe kwenye benki

Watu wakipiga foleni nje ya benki
Image caption Watu wakipiga foleni nje ya benki

Nyota wa filamu nchini India amezua hisia baada ya kupigwa picha akiwa amesimama katika foleni nje ya benki akiwa amebeba mwana wa nguruwe.

Ravi Babu amesema kuwa nguruwe huyo atashiriki katika filamu yake mpya kwa jina Adhigo ikimaanisha kutoka Telugo hadi ''there''.

Milolongo mirefu ya benki imekuwa kitu cha kawaida baada ya noti za rupee za 500 na 1000 kupigwa marufuku nchini humo katika vita dhidi ya ufisadi.

''Nilikuwa nikimpeleka ili kupigwa picha nilipogundua kwamba sina fedha za mafuta'',Babu aliambia BBC.

Image caption Ravi Babu akibeba mwana wa nguruwe

''Nilisimama katika eneo la ATM lakini nikalazimika kumbeba mimi mwenyewe baada ya kupiga kelele wakati msaidizi wangu alipojaribu kumbeba.Lazima umbebe ikiwa mkono wako uko katika kifua chake na umuweka karibu nawe ili ajihisi vyema''.

Picha hiyo imesambazwa katika mitandao ya kijamii nchini India.

kumekuwepo na visa vya ghasia nchini India tangu marufuku hiyo ya noti itangazwe ikiwa ni miongoni mwa harakati za kukabiliana na ufisadi wiki mbili zilizopita.

Watu wamekuwa wakipiga foleni kwa saa kadhaa nje ya benki pamoja na mashine za ATM ambazo huenda zikaishiwa na fedha.

Hatua hiyo imeathiri uchumi wa India.