Waziri ahamia katika nyumba yenye choo cha kuzuia risasi India

Jumba la waziri mkuu wa Telangana nchini India
Image caption Jumba la waziri mkuu wa Telangana nchini India

Waziri mkuu wa jimbo la Telangana nchini India amezua hisia baada ya kuhamia katika nyumba mpya inayogharimu walipa kodi dola milioni 7.3.

Jumba hilo lina ukubwa wa mita 9,000 mraba katika mji wa Hyderabad.

Image caption Jumba la waziri mkuu wa Telangana nchini India

Nyumba hiyo ina vyoo vilivyo na uwezo wa kukinga risasi kuingia, ukumbi ulio na viti 250 na eneo la mikutano linaloweza kuingiza watu 500.

Jumba hilo lilibarikiwa na mshauri wa maswala ya kidini wa waziri huyo huku choo hicho kinachoweza kuzuia risasi kuingia kikifanyiwa masikhara.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Baadhi ya maoni yaliochapishwa katika mtandao wa Twitter

Waziri mkuu K Chandrashekhar Rao alihamia katika jumba hilo siku ya Alhamisi baada ya msururu wa matambiko ya kidini yalioongozwa na mshauri huyo wa maswala ya kidini Chinna Jeeyar Swamy.

Bw Swamy pia aliketi katika kiti rasmi cha bw Rao ili kukibariki.

Image caption kabla ya waziri huyo kuhamia jumba hilo tambiko la kidini lilifanywa

Jumba hilo kwa jina Pragathi Bhavan lilijengwa kwa ushirikiano wa vaastu.