Sudan Kusini yaafiki kutumwa kwa walinda amani wa kikanda

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir

Sudan Kusini imekubali kutumwa mara moja kwa kikosi cha kikanda kuboresha zaidi shughuli za kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa. Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini wamekuwa wakishutumiwa kwa kushindwa kuwalinda raia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kikosi cha Afrika cha kikanda kitakuwa na majukumu zaidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa walioko huko

Kikosi imara cha wanajeshi elfu nne kitakuwa na ngome yake katika mji mkuu Juba na kitakuwa na majukumu zaidi ya kikosi cha Umoja wa Mataifa.

Awali Sudan Kusini South iliweka masharti magumu kuhusu muundo wa kikosi hicho. Mapigano makali yalizuka mjini Juba mwezi wa Julai.

Taifa la Sudan Kusini limekuwa likiathirika na mzozo tangu mwaka 2013 ,miaka miwili baada ya kupata uhuru kutoka Sudan.