Conte: Chelsea ni timu tofauti sasa

Antonio Conte
Image caption Antonio Conte

Viongozi wa ligi ku ya Uingereza Chelsea ni timu tofauti na ile ilioanza msimu,lakini ni sharti inyenyekee,mkufunzi wake Antonio Conte amesema.

Timu hiyo iliishinda Tottenham Hotspurs 2-1 katika uwanja wa Stamford Bridge hivyobasi kujipatia ushindi wao 7 mfulululizo.

Ushindi huo umeimarisha uongozi wa klabu hiyo katika kilele cha ligi.

Nadhani sasa tuna timu tofauti, tuna motisha tofauti, na ni muhimu kuendelea kuwa wanyenyekevu, alisema Conte.

Unaposhindwa debi muhimu,lazima ufurahie lazima tuendelee kufanya kazi.