Phyllis Wakiaga: Mwanamke aliyefana katika usimamizi Kenya

Phyllis Wakiaga: Mwanamke aliyefana katika usimamizi Kenya

Phyllis Wakiaga ni Afisa Mkuu Mtendaji wa Chama cha Watengenezaji Bidhaa Kenya (KAM). Tangu akiwa mdogo, alikuwa na ndoto ya kuwa afisa mkuu mtendaji.

Azma yake kuu ni kutaka kuona mabadiliko katika fikira, tabia na uongozi nchini Kenya.

"Ninafanya kazi ya kuhakikisha kuwa tuna mabadiliko ambayo yanaweza kufanya biashara zetu ziwe, ili tuweze kuunda nafasi za ajira na kuwaajiri vijana wetu,” anasema.