Mwanamke aliyeacha ulevi baada ya miaka mingi Kenya

Idadi ya wanawake wanaotumia pombe inazidi kuongezeka nchini Kenya. Patricia Gachuki ni mmoja wao lakini hatimaye aliamua kuiacha na kuingilia ukulima. John Nene ametuandalia ripoti hii baada ya kuzungumza naye akiwa kwenye shamba lake mtaa wa Shela, kisiwa cha Lamu.