Mfalme Charles Mumbere afunguliwa mashtaka

Charles Mumbere alitawazwa kuwa mfalme wa Rwenzururu mwaka 2009
Image caption Charles Mumbere alitawazwa kuwa mfalme wa Rwenzururu mwaka 2009

Charles Wesley Mumbere, ambaye ni mfalme kutoka magharibi mwa Uganda amefunguliwa mashtaka ya mauaji kufuatia mapigano ya mwishoni mwa wiki ambapo utawala unasema kuwa watu 62 waliuawa.

Anatawala katika ufalme ya kitamaduni kwenye milima ya Rwenzori umbali wa kilomita 340 magharibi mwa mji mkuu Kampala.

Wafuasi wake ambao ni jamii ya Bakonzo wamesambaa kutoka nchini Uganda hadi nchi jirani ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa msukosuko umekuwa mkubwa kwenye ufalme huo miaka ya hivi karibuni.

Mizozo ya ardhi imesababisha migawanyiko kuhusu mipango ya kuigawanya kasese, moja ya wilaya saba zilizo eneo la Rwenzori.

Sasa mfalme Mumbere na baadhi ya wafuasi wake wamelaumiwa kwa kupanga kubuni vuguvugu la kujitenga na kuunda taifa jipya kwa jina Yiira.

Hata hivyo ufalme huo umekana madai hayo.

Charles Mumbere alitawazwa kuwa mfalme wa Rwenzururu mwaka 2009, bbada ya kuishi na kufanya kazi nchini Marekani kwa miaka mingi.