Kocha Barry Bennell apata ahueni

Uingereza
Image caption Kocha Barry Bennell apata ahueni

Kocha wa zamani wa soka Barry Bennell ameshtakiwa kwa makosa nane ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya kijana mwenye umri chini ya 14, waendesha mashitaka wameeleza.

Waendesha mashtaka kutoka Crown, wameeleza kuwa wamepokea jalada lenye ushahidi kutoka polisi wa Cheshire kuhusiana na madai ya unyanyasaji wa kihistoria.

Kocha Bennell ambaye kwa sasa ana umri wa miaka sitini na mbili, ambaye awali alikuwa kocha wa timu ya vijana ya Crewe Alexandra, na kwamba atahitajika kufika mahakamani mnamo Decemba kumi na nne.

Mashtaka yanayomkabili yanadaiwa kutendwa na kocha huyo kwamba yalitendwa kati ya miaka ya 1981 na 1985.

Ikumbukwe kwamba Bennell alikutwa akiwa hajitambui huko Knebworth Park, Stevenage,baada ya kutoonekana hadharani na kupelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi, na inaarifiwa kuwa baada ya kupatiwa matibabu kwa sasa afya yake imeimarika na ameruhusiwa na afya yake inazidi kuimarika.