Kumbi za filamu kucheza wimbo wa taifa India

Wimbo wa taifa nchini India kuchezwa katika kumdi za kuonyesha filamu Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wimbo wa taifa nchini India kuchezwa katika kumdi za kuonyesha filamu

Mahakama ya juu nchini India imetoa uamuzi kwamba nyimbo ya taifa ni sharti ichezwe katika kila ukumbi wa filamu kabla ya filamu kuanza.

Majaji wamesema kuwa agizi hilo ni sharti kutekelezwa katika kipindi cha siku 10 .

Watazamaji watalazimika kusimama wakati wimbo wa taifa unapochezwa.

Mnamo mwaka 1960 na 1970 ,kumbi za filamu zilikuwa zikicheza wimbo huo lakini hatua hiyo ikaIemazwa baada ya watazamaji kutosimama ama hata kuondoka katikati ya wimbo huo unapochezwa.

Hakuna sheria ya moja kwa moja kuhusu nyimbo hiyo ya taifa na kwamba majimbo mengi yamekuwa huru kuchagua sheria zao.

Mwaka 2003, jimbo la magharibi la Maharashtra lilizilazimu kumbi za filamu kucheza wimbo huo, lakini mwaka uliopita,mahakama ya Madras iliamua kwamba ni lazima kusimama wakati wimbo huo unapochezwa.

Siku ya Jumatano,majaji hao waliamua kwamba ni lazima wimbo wa taifa kuchezwa katika kumbi za filamu mbali na kuonyesha picha ya bendera wakati wimbo huo unapochezwa.