Serikali yatoa ufafanuzi kuhusu masomo maalum Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Serikali yatoa ufafanuzi kuhusu masomo maalum Tanzania

Kwa takribani siku nne sasa, nchini Tanzania kumekuwa na mjadala mkali juu ya hotuba ya waziri wa elimu wa nchi hiyo kuhusiana na taratibu za udahili wa wanafunzi katika vyuo Vikuu.

Sehemu ya hotuba ya waziri huyo wa Elimu ilikuwa inaukosoa utaratibu wa vyuo vikuu kutoa mafunzo ya muda maalumu yaani foundation course kumuandaa mtu ambaye hakutimiza vigezo hapo awali ili kujiunga na masomo ya chuo kikuu.

Mwandishi wetu Arnold Kayanda amefanya mazungumzo na naibu waziri wa elimu wa Tanzania muhandisi Stellah Manyanya ili kupata undani wa tamko hilo