Ripoti: Silaha kutoka Iran, Korea na Urusi zinauzwa Yemen na Somalia

Uchunguzi uliofanyiwa silaha zilizoshikwa nchini Yemen, unaonyesha ushirikiano wa silaha uliopo kati ya Iran, Somalia na Yemen.
Maelezo ya picha,

Uchunguzi uliofanyiwa silaha zilizoshikwa nchini Yemen, unaonyesha ushirikiano wa silaha uliopo kati ya Iran, Somalia na Yemen.

Kati ya mwezi Februari na machi mwaka 2016, meli za kivita zikiwemo za HMAS Darwin, FS Provence na USS Sirocco, zilizokuwa zikihudumua kama kikosi cha kimataifa, zilishika mashua tatu zilizokuwa zikisafirisha silaha katika habari ya Arabia.

Mashua hizo zilikuwa na bidhaa zingine nyingi za kijeshi zinazokisiwa kutokea nchini Iran na zilozonuiwa kufika nchini Somalia na Yemen.

Ushahidi uliotokana na uchunguzi uliofanywa, na pia uchunguzi uliofanyiwa silaha zilizoshikwa nchini Yemen, unaonyesha ushirikiano wa silaha uliopo kati ya Iran, Somalia na Yemen.

Barabara hii inakisiwa kutumiwa kusafirisha idadi kubwa ya silaha zilizotengezwa nchini Iran huku zikilengwa kusafirishwa hadi nchini Somalia na Yemen.

Wahudumu kutoka meli za FS Provence na HMAS Darwin wote walipata bunduki za rashasha zinazokisiwa kutengezwa nchini Korea Kaskazini. Silaha zilizokuwa na namba sawa zilipatikana ndani ya vyombo viwili tofauti ishara kuwa silaha hizo zilitoka eneo moja.

Vikosi kutoka milki ya nchi za kiarabu vinadai kukamata silahaha nchini Yemen, zikiwemo zile zilizotengezwa nchini Iran na Urusi.