Walinzi wa mfalme waliwaua polisi 16 Uganda

Image caption Mfalme Charles analaumiwa kwa kutaka kubuni taifa huru

Maiti za polisi wa Unganda waliouawa wakati wa mapigano na walinzi wa mfalme wa Rwenzururu Magharibi mwa Uganda eneo la Kasese zimesafirishwa kwenda kituo kikuu cha polisi eneo hilo.

Msemaji wa polisi Andrew Felix Kaweesi, aliwaambia waandishi wa habari kuwa watu 62 waliuawa wakati wa mapigano hayo mwishoni mwa wiki.

Image caption Jumla ya polisi 16 waliuawa kwenye mapigano

Ripoti zingine zinasema kuwa watu 82 waliuawa wakiweme polisi16 pamoja na walinzi wa mfalme.

Mfalme Charles Mumbere alikamatwa baada ya vikosi vya serikali kuvamia makao yake siku ya Jumamosi.

Image caption Ghasia zilizuka eneo la Kasese magharibi mwa Uganda

Ameshtakiwa kwa makosa ya maujai ya polisi mwezi Machi na wala si kutokana na sababu ya ghasia za mwishoni mwa wiki.

Mfalme Charles amekana kuhusika kwenye ghasia hizo.