Kanye West aondoka hospitalini

Image caption Kanye West alipatwa na tatizo la uchovu

Mwanamuziki Kanye West anaripotiwa kurejea nyumbani zaidi ya wiki moja baada ya kulazwa kutokana na uchovu.

Kulingana na taarifa tofauti nchini Marekani, mwanamuzi huyo aliondoka hospitali ya UCLA jimbo la Los Angels na mkewe Kim Kardashian pamoja na daktari wake Michael Farzam,

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kanye alilazwa hospitali ya UCLA jimbo la Los Angels

Kanye West mwenye umri wa miaka 39 alilazwa hospitalini siku ya Jumatatu bada ya kupatwa na uchovu uliotokana na kukosa usingizi na kuishiwa na maji mwilini, kwa mjibu wa TMZ.

Nalo jarida la People limenukuu taarifa zinazo sema kuwa Kanye yuko nyumbani akiwa anapumzika.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kanye West alisitisha kwa ghafla tamasha lake

Alitumia karibu muda wa dakika kumi akizungumza kuhusu Beyonce, Jay Z, Hillary Clinton na mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerbrg wakati kifanya shoo.

Mwanamitindo Kendal Jenner, ambaye ni dada wa kambo wa Kim Kardashian, alisema kuwa familia imekuwa ikimuombea Kanye.