Asilimia 99 ya chaja bandia za Apple haziko salama

Asilimia 99 ya chaja za Apple haziko salama Haki miliki ya picha AP
Image caption Asilimia 99 ya chaja za Apple haziko salama

Wachunguzi wamewaonya wateja kuwa wanakabiliwa na hatari kubwa baada ya kubainika kuwa asilimia 99 ya chaja bandia za vifaa vya Apple haziko salama.

Wakaguzi wa viwango vya bidhaa wamesema kuwa vifaa bandia vya kielektroniki ni vingi mno.

Kati ya chaja 400 bandia ,ni nne pekee zilizopatikana na kinga dhidi ya umeme.

Tangazo hilo linajri wakati ambapo Apple imelalamika kuhusu vifaa bandia vinavyouzwa kwa kutumia jina lake.

Apple ilifichua mnamo mwezi Oktoba kwamba ilikuwa inamshtaki muuzaji fulani ambaye ilidai anahatarisha maisha ya wateja wake kwa kuwauzia vifaa vya kudhibiti moto kwa kutumia jina lake.

Vipimo hivyo vya viwango vilifanywa na wataalamu wa usalama.

Walitumia moto mwingi kukagua chaja hizo zilizonunuliwa mtandaoni kutoka mataifa manane ikiwemo Marekani ,China na Australia ili kubaini iwapo zina kinga ya umeme.