Wasifu wa rais mteule wa Gambia Adama Barrow

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Adama Barrow
  • Adama Barrow alizaliwa mwaka 1965 katika kijiji kimoja karibu na mji wa kibiashara wa Basse Mashariki mwa Gambia.
  • Alihamia mjini London miaka ya 2000 ambapo anaripotiwa alifanya kazi kama mlinzi kwenye duka moja, Kaskazini mwa London, akiendelea pia na masomo yake.
  • Alirejea nchini Gambia mwaka 2006 ambapo alianzisha kampuni yake ya kuwekeza.
  • Barrow mwenye umri wa miaka 51 aliteuliwa kuongoza muungano wa vyama saba vya upinzani kumpinga Rais Yahya Jammeh.
  • Amekosoa kutokuwepo kwa miula miwili kwa urais na pia kulaani kufungwa kwa wanasiasa wa upinzani.
  • Anaunga mkono uhuru wa mahakama, wa vyombo vya habari na wa vyama vya umma.