Trump awasasiliana na Rais wa Taiwan

Haki miliki ya picha AP
Image caption Trump alituma ujumbe kupitia Tweeter akisema amepigiwa simu na kiongozi wa Taiwan, Mama Tsai Ing-wen

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amekiuka utaratibu wa miongo kadhaa kwa kuwasiliama moja kwa moja kwa simu na Rais wa Taiwan, hatua inayoweza kuvuruga uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Uchina.

Kundi la Trump linaloshughulikia maswala ya kupokezena uongozi kutoka kwa Rais Barack Obama, lilisema kuwa viongozi hao wawili walijadiliana maswala ya kiuchumi na usalama kati ya Marekani na Taiwan.

Bwana Trump baadaye alituma ujumbe kupitia Tweeter akisema kuwa amepigiwa simu na kiongozi wa Taiwan, Mama Tsai Ing-wen. China inatambua eneo hilo linalojitawala lenyewe kama sehemu moja ya taifa lake.

Marekani ilivunja uhusiano wa kidiplomasia ya Taiwan mwaka 1979.

Utawala wa Rais Tsai haitambui madai ya China kuwa wao ni sehemu yake, hatua ambayo imesababisha Uchina kusitisha aina yo yote ya mawasiliano na kisiwa hicho.

Ikulu ya White House hadi sasa inatambua Taiwan kuwa sehemu moja ya Uchina.