Barrow: "Hii ni Gambia mpya"

Adama Barrow alipata kura 263,515

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha,

Adama Barrow alipata kura 263,515

Rais Mteule wa Gambia, Adama Barrow, ametaja kile alichosema ni "Gambia Mpya" kufuatia ushindi wake wa kushangaza dhidi ya Yahya Jammeh, aliyenyakua madaraka mwaka 1994 kwa mtutu wa Bunduki.

Bwana Barrow, aliyekuwa wakati mmoja mfanya biashara wa kujenga na kuuza nyumba ambaye hana ujuzi wowote wa kisiasa, ameshangazwa na ushindi wake.

Bwana Jammeh amekosolewa na makundi mengi ya haki za kibinadamu kwa ukiukaji wa haki za raia nchini, alisema kuwa Allah alikuwa akimweleza kuwa muda wake umekamilika.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Watu wakishangilia Banjul

Alisema hatapinga matokeo ya uchaguzi na kwamba ananuia kurudi shambani mwake baada ya kukabidhi madaraka Januari, mwaka ujao.

Maelfu ya wakaazi wa mji mkuu wa Banjul walijitokeza barabarani na kusherehekea matokeo hayo.