Urusi yadai kumuua kiongozi wa Islamic State

Wanajeshi maalum wa Urusi Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi maalum wa Urusi

Maafisa wa usalama wa Urusi wamesema kuwa wameua kiongozi wa Caucasus wa kundi la Islamic State.

Maafisa wa idara ya ujasusi ya Urusi walimtaja marehemu kama Rustam Aselderov.

Inasemekana alikuwa mmoja wa wapiganaji watano waliouawa katika makabiliano kati ya kundi hilo na maafisa wa usalama katika wizara ya usalama wa nchi katika eneo la Makhachkala katika mji mkuu wa Dagestan.

Wasemaji wa jeshi la Urusi walisisitiza kuwa wapiganaji hao walishiriki katika uandalizi wa matukio kadhaa ya mashambulizi ya kigaidi, kukiwemo moja baya sana katika mtandao wa usafiri katika mji wa kiviwanda wa Volgograd.